viongozi watajika pamoja na wakenya wa tabaka mbalimbali wamejitokeza kuhudhuria mazishi ya msanii mtajika wa benga  Joseph Kamaru leo yaliyofanyika Muthithi PCEA Secondary School , Kigumo eneo bunge la Murang’a.

Kamaru aliaga dunia alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya MP Shah  Octoba tarehe 3, 2018 akiwa na umri wa miaka 79. Hadi kufikia kifo chake, alikuwa ametunga zaidi ya nyimbo elfu mbili.

Rais Uhuru Kenyatta, naibu Rais William Samoei Arap Ruto na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga wamemsifia kutokana na weledi wake kimuziki pamoja na kuunganisha jamii.

wasanii lukuki walijitokeza kumpumzisha mlezi wao.

 

 

Share.

About Author

Leave A Reply