Mwanahabari tajika Vincent Voiyoh amegura Qwetu radio. Mwanahabari huyo ameongeza orodha ndefu ya wanahabari na washika dau ambao wamegura chombo hicho cha habari ambacho kinakisiwa kusuasua kifedha.

Vincent Ateya ambaye alikuwa akifanya kipindi cha Qwetu asubuhi alihamia Royal media kufanya Jambo Kenya ya radio citizen, Selly Kadot Amutabi pia alihamia Royal media ambapo anafanya vipindi vya injili radio citizen. Wengine ambao hawapo tena ni radio ni Maureen Medza, Diblo Kaberia miongoni mwa wengi wengineo.

Hadi kugura kwake, Voiyoh alikuwa akifanya Qwetu Jioni na vipindi vya spoti. Vincent amehamia milele ambapo ataenda kuimarisha kikosi cha spoti ambacho kinahusisha Paulo Muchesi, Kaka Zema, Kelvin Kuria  na Mercy Mmbone.

Share.

About Author

Leave A Reply