Kama kutongoza vyeti,
Una zero kwa kabati,
Uvae na minisketi,
Mimi kwako hunivuti,
Hata vibaya ukiketi,
Huamshi mtu kati,
Umechina kijakazi.

Umechina kijakazi,
Mapenzi si yako kazi,
Kazi yako ni malezi,
Na kuupika mchuzi,
Kuparamia mnazi,
Inahitaji ujuzi,
Hata walio kwa ndoa….

Hata walio kwa ndoa,
Macho wawakonyezea,
Au hudhani najua,
Fulani wamumegea,
Yataja kutoka pua,
Kwa kutia ndoa doa,
Starabika kijakazi.

Share.

About Author

Leave A Reply