Uchunguzi wa DNA umedhibitisha kuwa wasichana wawili wanaofanana kama shilingi kwa ya pili; Sharon Lutenyo na Melon Mathias ni pacha wa Rosemary Khavareri .

Mwezi wa Aprili mwaka huu, pacha hao walizua gumzo, baada ya Sharon na Melon kufanana kiasi cha kuibua maswali miongoni mwa wanaowafahamu.

Wasichana hao ambao wana umri wa miaka kumi na tisa sasa, walizaliwa katika Hospitali ya Rufaa mjini Kakamega kisha wakatenganishwa katika hali tatanishi lakini wakaja kukutana ukubwani.

Walipokutana katika hafla iliyokuwa imeandaliwa katika shule ya Shikoti, wanafunzi wa shule walishangazwa na jinsi wawili hao walivyorandana.

“Nikiwa katika shule ya Shikoti, wanafunzi walianza kunicheka pindi waliponiona. Nilikuwa mwingi wa woga baada yao kuniarifu kuwa nilikuwa na dada tuliyefanana katika shule yao. Niliwafichulia kuwa nilikuwa na dada aliyekuwa akisoma katika shule ya upili ya Kimosin wala sio Shikoti,”Melon alisema.

Walianza urafiki Facebook mengine yote yakawa historia.

 

 

Share.

About Author

Leave A Reply