Mawaziri wanne walioamrishwa kufika mbele ya makao makuu ya upelelezi kurekodi taarifa kwa madai kuwa wanapanga njama ya kumuua Naibu Rais William Ruto wamekana madai hayo. Wanne hao ambao ni  Waziri wa afya Sicily Kariuki, waziri wa Kilimo Mwangi Kiunjuri , Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia Joe Mucheru na Waziri wa biashara na viwanda Peter Munya wamekubali kuwa wamekuwa wakikutana lakini kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya mlima kenya.

“DCI imetuthibitishia kuwa Naibu Rais William Ruto alilalama kuwa baadhi ya mawaziri wamekuwa wakikutana katika hoteli ya La Mada wakipanga njama ya kumuangamiza, ni kweli tulikutana ila hatupangi njama ya kumuungamiza yeyote,” Munya alisema kwa niaba ya wanne hao.

Share.

About Author

Leave A Reply