Baada ya nguri wa usomaji habari Omondi Job Onyango kugura Qwetu radio ambapo alikuwa mhariri wa taarifa, aliyekuwa msomaji wa habari radio citizen Jilani Wambura anakisiwa kuridhi mikoba yake.

Kupitia mtandao wake wa facebook Omondi Job Onyango ametangaza kuwa amegura Qwetu radio na kuhamia Milele FM ambapo atakuwa akisoma taarifa za habari kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne kuanzia tarehe mosi Julai. Ikumbukwe kuwa OJO aligura Milele fm Qwetu radio ilipokuwa ikianza.

 

 

Share.

About Author

Leave A Reply