Mahitaji

Mchele vikombe vitatu

Nyama kilo moja

Pilipili boga moja

Nyanya 2 kubwa

Vitunguu maji viwili

Kitunguu saumu iliyosagwa kijiko kimoja cha supu

Tangawizi kijiko kimoja cha chai

Ndimu moja

Mafuta ya kupikia nusu kikombe

Mdalasini nusu kijiko cha chai

Binzari nyembamba  kijiko kimoja cha chai

Pilipili manga  Kijiko nusu cha chai

Hiliki Kijiko nusu cha chai

 

Namna ya kutayarisha na Kupika

Roweka mchele wako katika chombo

Chukuwa nyama na ioshe vizuri na itie thomu, tangawizi, ndimu, pilipili manga na chumvi kiasi

Iweke jikoni hadi ikauke maji na kuwa imewiva huku ukiikaanga kaanga kwa hayo hayo mafuta yake hadi kuwa rangi ya hudhurungi

Katakata Vitunguu na nyanya weka pembeni

Chukua pilipili boga, thomu, tangawizi na visage katika mashine ya kusagia

Weka sufuria pembeni na utie mafuta, subiri yapate moto

Kisha tia vitunguu na vikaange hadi kuwa hudhurungi na tia nyanya

Kisha mimina mchanganyiko wako ulio usaga wa pilipili boga, thomu na tangawizi

Koroga kwa dakika kadhaa Kisha mininia nyama uliyokuwa tayari, maji kiasi na chumvi wastani na subiri maji hayo yachemke

Weka mchele humo na koroga kiasi na onja chumvi kama ipo sawa au kama ndogo unaweza kuongeza

Funika na punguza moto na uache uive taratibu

Baada ya kukauka maji kabisa basi ugeuze na subiri tena kwa dakika kama mbili na tayari kuliwa.

 

credit:http: mapishimatamu.blogspot.com

Share.

About Author

Leave A Reply