Kitendawili kigumu cha atakapozikwa Ken Okoth ambaye hadi mauti kumfika alikuwa mbunge wa Kibra kimegubika familia huku kukiwa na pande tatu kinzani.

Upande ‘moja unapendekeza Ken azikwe katika ardhi ya marejemu baba yake Nicholas Obonyo katika eneo linalofahamika kama Rangwe, Homabay huku upande wa mama Ken ambaye anafahamika kama Angeline Ajwang’ wakipinga pendekezo hilo kwa kuwa mama na baba ya Ken walitengana Ken akiwa mdogo na kulelewa na mama yake kitu ambacho kinapelekea wao kusema kuwa Ken anafaa kuzikwa katika shamba la upande wa familia ya mama.

Mke wa Ken kwa upande wake anasema kuwa Ken anafaa kuchomwa kama alivyopendekeza siku za uhai haki. Hata hivyo familia ya upande wa baba kupitia kwa msemaji wake Raymond Mbai wamepinga wakisema kuwa kuchomwa ni kinyume na tamaduni.

Uongozi wa chama cha ODM wakiongozwa na kinara Raila Odinga wamesema kuwa hawataingilia na kuachia familia kufikia uamuzi wa atakapozikwa na atakavyozikwa.

Huku haya yakijiri, mwanamke ambaye ni mwakilishi wadi mteule wa chama cha jubilee amejitokeza na mtoto wa miaka mitano na kudai kuwa Ken Okoth ndiye baba wa mtoto huyo na kuomba familia kutomtenga mwanawe wakati tangazo la kifo cha Ken litawekwa gazetini jumatano ya juma lijalo. Japo mama Ken awali alikuwa amepinga uwezekano wowote wa Ken kuwa na mke wa pili, duru za kuaminika kutoka kwa familia zinasema kuwa Ken alikuwa anampenda mwanawe huo na hata alikuwa akimtembelea mara kwa mara hadi kufikia kiwango cha kumgawia uridhi.

 

Share.

About Author

Leave A Reply