Kamene Goro ni mojawapo ya wanahabari tajika wa karne hii. Majina kamili anafahamika kama Michelle Kamene Goro .

Alizaliwa 24 March 1992.

Alisomea Rusinga international school kisha kujiunga na chuo kikuu cha Nairobi kusomea sheria lakini katika mwaka wa tatu akaanza kutia guu  bahari ya uanahabari

Alianzia taaluma ya uanahabari Ebru TV akiwa na umri wa miaka 21. Aliondoka Ebru 2017.

NRG Radio ilipofunguliwa, Kamene Goro alikonga nyoyo za watu alipoanza kufanya kipindi cha asubuhi kutoka saa kumi na mbili hadi saa nne pamoja na Andrew Kibe.

Kwa sasa Kamene anafanya kazi katika kituo cha radio cha Kiss fm Kenya lakini kuna mgogoro wa kimkataba na kituo cha NRG.

Amevuma sana kutokana na umbo lake la nane, uwezo wa kufanya kazi kwa radio na TV na kusema kama mambo yalivyo bila uoga. Kwa mfano, alikuwa gumzo mitandaoni 2018 alipokiri kuwa ameshiriki tendo la ndoa na wanaume ishirini na saba. Alikuwa gumzo pia wakati uhusiano wake na mpenzi wake mtanzania ulipoingia doa na kukiri hadhrani kuwa aliachwa kupitia ujumbe wa whatsapp siku chache kabla ya harusi.

Kamene ameingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kwa kuwa mwanahabari mchanga zaidi kusoma taarifa za habari Kenya.

Kamene anasema hana mpango wa kufunga ndoa au hata kupata watoto lakini likija likaja kutokea haidhuru!

 

 

Share.

About Author

Leave A Reply