John Ng’ang’a  maarufu kama John Demathew alizaliwa Gathiruini Mukurwe, Gatanga katika kaunti ya Muranga tarehe mosi juni 1967

Alisomea katika shule ya Mukurweini ambayo kwa sasa inajulikana kama Githambia Primary kisha kujiunga na shule ya upili ya Naru katika eneo bunge la Kandara na kuhitimishia Igikiro .

John Demathew alitunga wimbo wake wa kwanza akiwa darasa la saba kama anavyoeleza

Nilitunga wimbo wangu wa kwanza nikiwa darasa la saba ambao unafahamika kama rekereria wende tafsiri yake ikiwa achiliwa upendo. Kuna malimu alinitandika sana baada ya kutunga wimbo huo. Hamna hata mzazi mmoja wangu alipendezwa na mimi kujiunga na tasnia fya uimbaji. Hata kuna kipindi babangu karibu anifukuze nyumbani.

Baada ya kuhitimisha masomo yake ya upili, John alielekea Jiji la Nairobi ambapo alikuwa akiuza mboga sokomjinga na kisha kufungua butchery kariobangi na baadae kuhamia Nakuru alikokuwa akiuza viatu.

Kuna kaka zangu walikuwa na biashara Kariobangi nikaja kwao kuuza sukumawiki sokomjinga kisha nikafungua butchery Kariobangi na kisha nikahamia Nakuru kuuza viatu za plastiki ambazo zilikuwa zikifahamika kama Sadak tukuwa na msanii Sammy Muraya

Demathew alibahatika kukutana na wasanii kama vile Timona Mburu na Joseph Wamumbe ambao walimshika mkono akarekodi wimbo wake wa kwanza Jennifer mwaka wa elfu moja mia tisa themanini na sita.

Albert Gacheru maarufu kama wamaitu na wamumbe  walinisaidia sana kwa kunielekeza kipi cha cha kuimba na kipi si cha kuimba na ndipo nikafanikiwa kurekodi wimbo huo unaofahamika kama Jennifer …….

Hadi kufikia kifo chake, John alikuwa ameimba zaidi ya nyimbo mia tatu na hamsini lakini wimbo ambao ulimpatia umaarufu ni wimbo Peris Nduku aloimba mwaka wa elfu  moja mia tisa na themanini na saba.

Jamii ya Agikuyu wanaamini kuwa John hakuwa msanii tu bali pia alikuwa nabii na mengi aliyoyaimba katika siku za nyuma mengi yamekuja kutokea.

Kabla ya kupatwa na mauti, Demathew alikuwa ameunganisha wasanii na kutengeza sacco inayofahamika kama talented musicians and composers TAMCO ikiwa na malengo ya kuwasaidia wasanii kujiendeleza.

Tulianzisha TAMCO sacco ili wasanii wawekeze pesa zao ili wakija kuomba mikopo wasiulizwe una utajiri gani bali waulizwe umefikisha wapi sanaa.wasihangaike wanapotaka kununua vitu kama shamba au hata kujenga. Hatutaki kamwe kuzika wasanii wakipatwa na mauko kama bado ni masikini

Demathew alifarikia tarehe kumi na nane Agosti mwaka wa elfu mbili kumi na tisa baada ya kugonga trela Thika road karibu na hoteli ya blue post.

Katika mazishi yaliyofanyika tarehe kumi ishirini na nne agosti, Rais uhuru Kenyatta, naibu wa rais William Samoei Arap Ruto walikuwa miongoni mwa watu wengi waliohudhuria

John ameacha wake wawili na watoto. Lala pema palipo na wema John Demathew

Share.

About Author

Leave A Reply