Miezi michache baada ya mwanabloga mashuhuri Denis Itumbi kuhusishwa na barua iliyodaiwa kuwa feki ambayo ilikuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ambayo ilikuwa ikikisiwa kuwa na ushahidi wa kuuliwa kwa naibu Rais Daktari William Ruto, Denis amejipata mahakamani tena baada ya mwanamke kuelekea mahakani akimhusisha na kesi ya kutelekeza mtoto wake.

Kupitia kwa wakili Enricah Dulo, Itumbi hajakuwa akitoa msaada wowote kwa mwanawe na hivyo kuomba mahakama kumlazima Itumbi awe akimtumia elfu hamsini za kulea mtoto.

Kulingana na wakili Dulo, Wawili hao walikuwa katika uhusiano baina ya Januari mwaka jana na Agosti ambapo Denis alikimbia baada ya msichana kumwambia alikuwa na uja uzito wake. Tangu hapo jitihada za mwanamke kumfikia Itumbi zikiambulia patupu.

Kesi imeratibiwa kusikilizwa tarehe ishirini na sita septemba.

Share.

About Author

Leave A Reply