Licha ya kuwa Kazungu hulemewa na kizungu kuliko kitu kingine chochote, alibahatika kutongoza msichana wa kizungu na kufanikiwa kile ambacho vijana wa kileo huita kuingiza mtu box.  Akawa gumzo la mjini haswa baina ya vijana wa rika lake. Si kanisani, si misikitini, si maeneo ya burudani, si hotelini, kote waliongea kuhusu uhodari wa Kazungu. Kile ambacho hawakukijua ni kuwa Kazungu alikuwa amezongwa na mizengwe.

Kila siku alitarajiwa kumpeleka mpenzi wake mlimani zaidi ya mara tano. Sio kumpeleka tu, la hasha. Alifaa amfikishe kileleni zaidi ya mara moja kila wakati. Tatizo kuu likiwa iwapo Kazungu angetokwa na jasho na kuishiwa na nguvu kabla ya kumfikisha mwenzake kileleni, alinuniwa na hata kutishiwa kuachwa.

Kadri siku zilivyosonga,  Kazungu aliendelea kukonda na kuchoka na safari za kukwea mlima hadi kileleni jambo ambalo lilimghasi sana mpenzi wake.

“Iwapo kesho hutanifikisha kileleni nitatatafuta mbadala”alisema msichana wa kizungu baada  ya Kazungu kuhema nusu ya safari.

Kazungu alijua vinywa vilivyomsifia vitanponda akitemwa zaidi ya zilivyomsifia na kutokana na hilo ikabidi  atafute mbinu mbadala  ambazo zingemfanya amfikishe mpenzi wake kileleni. Katika harakati  za kutafuta dawa mujarabu ya tatizo lake akapatana na mkuyati.

Kesho yake akanywa mkuyati na kumsubiri mpenzi wake ambaye hakuwahi kufika. Matatizo yalimzidi, damu ikachechemka na kufanya mguu wa kukwea mlima usisimke kuliko ulivyowahi kusisimuka katika historia ya maisha yake. Lazima kungefanyika jambo haraka la sivyo Kazungu angekata roho.

Mamake Kazungu alimpata mwanawe si wa maji si wa chakula, akamkimbiza hospitalini ambapo alikaribishwa na maneno ya daktari kuwa ili maisha ya Kazungu yaokolewe dawa ilikuwa moja: kukwea mlima. Mamake mtu akaokoa maisha ya mwanawe kwa kufanya kile tu kingefanywa kuokoa maisha ya mwanawe.

Kazungu alipokuja kugundua kuwa mamake ndiye aliokoa maisha yake kwa kumpeleka mlimani, akajitia kitanzi. Mamake mtu pia akafuata mkondo huo huo wa kujitia kitanzi.

Siku Kazungu na mama yake wanazikwa, msichana wa kizungu hakupata nafasi ya kuenda mazishi, alikuwa akipandishwa mlimani na mandume mawili katika mchezo ambao kawaida huwa wa watu wawili lakini kwa mtu kama msichana wa kizungu, hakuna ziada mbovu. Japo Kazungu shupavu wa methali alipo, alisahau methali inayosema kuwa kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake!

picha kwa hisani ya blackoutdoors.wordpress.com

 

 

 

 

 

 

 

Share.

About Author

Leave A Reply