Gavana wa Nairobi Mike Sonko atakuwa kwa debe ya urais 2022. Taarifa za kugombea kwake zilivunjwa na Livondo usiku wa tarehe 10/11/2019 alipokuwa wakihutubia wakaazi wa Narok. Gavana na kikosi chake walikuwa wakitoka hafla ya thanksgiving ya Don Bosco Gichana iliyokuwa ikifanyika Kisii ambayo pia iliunganishwa na hafla ya kuchangisha pesa za kujenga jengo Kisii university.

“Mumeona aliyofanyiwa Gavana wetu kule Nairobi ambaye ni Rais wetu 2022 na EACC…… ” Livondo

Livondo aliwaambia wakaazi wa Narok kuwa Gavana Mike anahangaishwa na ICC ili kuzima azma yake ya urais lakini hawatarusu na kuwarai wakaazi wawaunge mkono.

Sonko kwa upande wake, aliwakikishia wakaazi kuwa atagombea urais kwa kuwa yeye ndiye chaguo la kipekee ambalo linaelewa wananchi.

“Tukimalizia, si mnajua mimi ndiye Sonko wa Masonko duniani? (wanaanchi wanaaitikia)…………Mjue hii Kenya lazima kuwa na rais ambaye anawaelewa na huyo si mwingine bali ni sonko wa masonko duniani” Mike Sonko

Japo wachanganuzi wanasema kuwa siasa za Kenya ni za kikabila na ni vigumu  mtu kupata urais kama mtu hajazaliwa katika makabila ambayo yanaaminika kuwa na watu wengi, wengi wamesema kuwa mfumo wa Mike Sonko unaendana na mfumo anaotumia Donald Trump na hilo linaweza kufanya aibuke na ushindi kwa njia ya kushangaza kama alivyofanya rais wa marekani Donald Trump.

Share.

About Author

Leave A Reply