Rais wa marekani Donald Trump amepigiwa  kura ya kungatuliwa uongozini na bunge la congress kwa misingi ya matumizi mabaya ya madaraka na kujaribu kuzuia shughuli za bunge hilo kwa kutoshirikiana na bunge hilo. Hatua ambayo imefanya abaki na kigezo kimoja tu cha kuamua kama atangatuka ama atasalia uongozini; bunge la seneti.

Trump ni Rais wa tatu kupigiwa kura hio katika historia ya marekani: Andrew Johnson na Bill Clinton

Kura zote zilipigwa kulingana na mirengo ya vyama huku karibu wabunge wote wa chama cha Democtrats wakipiga kura kuunga mkono ashtakiwe huku mrengo wa Trump wa Republican wakipinga kura hiyo.

Wakati akipigiwa kura hio, Trump alikuwa akiwatubia wafuasi wake Michigan

 “Wakati tunabuni ajira na kupambana kwa ajili ya Michigan, wenye itikadi kali za mrengo wa kushoto katika Kongresi wamejawa na wivu na chuki na hasira kubwa, unaona kile kinachoendelea.” Donald Trump

Kura za matumizi mabaya ya mamlaka zilikuwa 230 ndiyo na 197 la na kuzuia utendaji wa wa bunge la congress zikawa 229 ndiyo na 198 La.

Japo hatua ya congress huenda ikaaathiri mchakato wa Trumph kugombea urais katika awamu ya pili, wachanganuzi wanaamini kuwa Trump atasalia madarakani kwa kuwa chama cha Republican ambacho kinaunga mkono Trump kina wawakilishi wengi katika Bunge la Seneti kwa hivyo anatarajiwa kushinda kesi hiyo na kusalia madarakani.

Share.

About Author

Leave A Reply