Wawakilishi wadi wa gatuzi la Kiambu wamemngatua Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu kwa madai ya kuvunja sheria ya ununuzi, kutumia pesa za umma vibaya na kutumia mamlaka yake visivyo.

Hii ni baada ya msuada uliowasilishwa katika bunge hilo na Mwakilishi Wadi Solomon Kinuthia wa Ndenderu kuidhinishwa na wabunge 63 kati ya 92. Kulingana na msuada wa Kinuthia, Waititu alikwenda kinyume na sheria za ununuzi kutumia pesa za umma, na kutumia mamlaka yake vibaya. Aliwapa zabuni kubwa watu wa familia yake miongoni mwa tuhuma nyingi nyinginezo.

Share.

About Author

Leave A Reply