Katika mkesha wa kukoga mwaka wa elfu mbili kumi na nane kuingia mwaka wa elfu mbili kumi na tisa, Ferdinand Waititu alitaja kuwa mwaka wa elfu mbili na ishirini kuwa mwaka ambao angeeleza ufanisi wake bila kujua safari yake ilikuwa inaelekea ukingoni

Waititu ambaye ni maarufu kwa jina la Baba Yao alizaliwa januari tarehe 1 mwaka wa 1962  na safari yake katika siasa ikaanza mwaka wa 2002  alipchaguliwa diwani wa Njiru  kupitia chama cha KANU .  Katika uchaguzi mkuu wa 2007 aliawania ubunge Embakasi  dhidi ya  kigogo  David Mwenje na  mwanasiasa  aliyekuwa mgeni  katika siasa za eneo hilo Meritus Mugabe Were .

Mugabe Were aliwashinda Waititu na Mwenje lakini akauliwa nje ya lango lake mtaani Woodley Januari tarehe 29 mwaka wa 2009 siku chache kabla ya kuapishwa kuwa mbunge.

Katika uchaguzi mdogo ulioafuatia  Waititu alinyakua ushindi na kateuliwa kuwa  wazri msaidizi katika serikali ya muungano .Baadaye alipokonywa wadhfa huo baada ya  kukabiliwa na madai ya uchochezi  . Mwaka wa 2013 Babayo aliamua kuwania kiti cha ugavana jijini Nairobi kupitia tiketi ya TNA  lakini akashindwa  na  Evans Kidero wa ODM.

Mwaka wa elfu mbili kumi na tano, aliyekuwa mbunge wa kabete kipindi hicho George Muchai aliuliwa na kusababisha uchaguzi mdogo kufanyika. Ni katika uchaguzi huo mdogo Waititu aliamua kugura Nairobi na kuelekea Kiambu kugombea ubunge wa eneo hilo na kufanikiwa kushinda kiti hicho.

Katika uchaguzi wa mwaka wa elfu mbili kumi na saba, Baba yao aliamua kugombea Ugavana kaunti ya Kiambu ambapo alimbwaga Gavana wa kipindi hicho William Kabogo.

 

Miezi michache baada ya kuapishwa kama gavana ,tofauti ikaibuka kati yake na naibu wake James Nyoro na washirika wake  kadhaa waliomsaidia kukishinda kiti hicho .

Madai ya ubatilifu wa pesa za kaunti yakamwandama. Masaibu yakaendelea kumwandama hadi kufikia wakati wabunge wa kaunti ya Kiambu walipopitisha hoja ya kumfurusha kwa tuhuma za kujinufaisha kutumia kandarasi ,utumizi mbaya wa fedha za umma na kutumia vibaya maamlaka ya afisi yake.

Babayao alipewa fursa kufika senate ili kujitetea dhidi ya madai hayo.Aliwaraia maseneta kumsaza na hata akaawambia siku moja watakuwa magavana na  yeye atakuwa seneta kwa hivyo wamhurumie lakini ng’o! Kauli ikawa kumwondolea jina la gavana na kumrejesha katika meza ya kujipanga upya . Hayajaishia hapo-Waititu yungali ana kesi ya kujibu kortini kuhusu madai yaliyotolewa na waakilishi wa kaunti ya Kiambu .

Alipopewa nafasi kujiteta na Maseneta, aliwarai maseneta kumhurumia kwa kuwa huenda kuna kipindi watakuwa magavana naye akiwa Seneta na huenda atawaonea Imani. Hata hivyo maseneta hawakusikia rai yake. Wakagongelea msumari wa mwisho katika jeneza, akavuliwa ugavana na aliyekuwa naibu wake James Nyoro akaapishwa kuwa Gavana wa Kiambu tarehe thelathini na moja Januari mwaka wa elfu mbili na ishirini.

Baba yao amekuwa gavana wa kwanza kungatuliwa ugavana tangu ugatuzi. Wadadisi wa kisiasa wanasema huenda huu ndio utakuwa mwisho wa Ferdinand Waititu kisiasa.

Share.

About Author

Leave A Reply