“Leo nataka niwambe mbinu zipi zilinisaidia mimi kufika hapa.

Mko tayari kusikia hizo mbinu?

Hadhira: Ndio

Mnataka kufanikiwa?

Hadhira: Ndio

Mnaamini kuwa wote tunaweza kufanikiwa?

Hadhira: Ndio

  1. Kutochagua kazi

Naomba mnisikilizeni. Cha kwanza kabisa ambacho kimekuwa msaada wangu ni kuto chagua kazi.

Mimi nilikuwa sichagui kazi yeyote. Wakati naanza Tandale huko kwanza, nakumbuka nilikuwa nabeba mchanga naenda kuuza kwa watu wanaojenga. Kuna kipindi nilikuwa nafanya kwa petrol station ya Shell  kuuza mafuta.

Kuna kipindi pia nilikuwa nauza nguo, Naamka alfajiri naenda Tandale sokoni nalenga, nikishalenga naanza kutembeza tembeza kwa watu nikiwauzia…….

Nikaendaaaa kuna kipindi nilikuwa napiga picha, nilikuwa nawahi haruhi, napiga kisha nawahi kuziprint Kariakor halafu nazitandaza pale nje nauza picha moja mia mbili.

  1. Ubunifu

Katika kufanya kazi kwangu nilijifunza ili ufanikiwa katika kazi zote lazimauwe mbunifu.

Unaweka ubunifu gani kuonyesha kuwa kutu chako kina dhamani?

 

  1. Uaminifu

Kitu kingine uaminifu, mtu akikupa kazi Senti yake ndogo unaitunza na kumfanyia kazi yake ipasavyo inafanya kukuamini na kesho na kesho kutwa kukupatia kazi nyingine

  1. Kuomba Mungu

Nakumbuka wakati katika hussle zangu Kaka Domomo aliwahi kuniambia hakuna kitu kinaleta mafanikio kama kumuomba Mwenyezi Mungu.

  1. Kutotumia mihadarati

Mihadarati inazidi kukudidimiza na kukufanya usifanikiwe. Mtu hawezi kukupatia kazi kama unatumia mihadarati kwa sababu anaona kuwa utamwibia yaani huaminiki.

Imani iliyotengenezeka ni kuwa Imani iliyotenenezeka na iliyokuwepo na ndio ya kweli ni kwamba anayevuta unga atakuwa mchukuzi.

Kama tunataka tunafanikiwe lazima tuache mihadarati. Kakangu Chidi Benz husema kuwa kitu ambacho kinakupa raha na kukuumiza sio kitu kizuri.

  1. Usikate tamaa

Usiogope kunyanyasika kwa sababu mtu hawezi kukusaidia kiwepesi lazima umuonyesha kuwa una nia”

Share.

About Author

Leave A Reply