Aliyekuwa rais wa pili wa  Kenya, Daniel Toroitich  Arap Moi ameaga dunia. Taarifa za kifo chake zimetangazwa na rais Uhuru Kenyatta na kuidhibitishwa na  msemaji wa familia hiyo Lee Kinyanjui alisema Moi alitangazwa kufariki na madaktari  asubuhi ya leo Jumanne, Februari 4. Amefariki katika Nairobi Hospital ambako amekuwa akitibiwa mara kwa mara.

Moi alichukua hatamu za uongozi kutoka kwa hayati mzee Jomo Kenyatta, mnamo mwaka 1978 na kuongoza taifa hili kwa miaka 24 kabla ya kuondoka madarakani mwaka 2002.

Mwenda zake alizaliwa mnamo Septemba 2, 1924, katika kijiji cha Kabarak , Wilaya ya Sacho Kaunti ya Baringo na kufariki tarehe 4 Fe bruari mwaka wa elfu mbili na ishirini akiwa na umri wa miaka 95.

Atakumbukwa kwa mengi ikiwemo maziwa ya nyayo ambayo yaliwafaidi wengi enzi wakisoma katika shule za msingi, msemo wake wa fuata nyayo na siasa mbaya maisha mbaya.

Share.

About Author

Leave A Reply