Usiku wa tarehe saba Februari mwaka wa elfu mbili na ishirini, mwili wa wa marehemu papa Denis ulipatikana Ngara akiwa na majeraha ya kile kilichodaiwa kuwa ama kuuliwa au kujiua.

Hujambo na karibu tujue kuhusu Papa Denis, alikozaliwa, alivyolelewa, alivyoingia katika tasnia ya muziki, utajiri wake wa haraka na mazingira tatanishi ya kifo chake.

Dennis alizaliwa Matunda, Mois bridge karibu na kitale eneo la magharibi mwa Kenya na kupewa jina Dennis Mwangi.

Alizaliwa katika familia ya watu watano na kulelewa na mama kwa kuwa babake alifariki Denis akiwa bado mchanga.

Akiwa katika darasa la nane, mama yake aliaga dunia na kufanya maisha yaliyokuwa magumu kuwa magumu zaidi. Papa Deno hakuweza kuenddelea na shule ya upili kwa sababu ya ugumu wa maisha lakini akaamua kujituma ili kumwelimisha kaka yake ambaye walizaliwa mapacha. Kando na kuzaliwa mapacha, wanafanana kama shilingi kwa ya pili.

Papa Denis aliwahi kufanya kazi nyingi ikiwemo kuwa hawker, kufungua video show miongoni mwa kazi nyingi nyinginezo.

Aliwahi kuhama matunda na kuelekea kisumu kutafuta maisha lakini vurugu za mwaka wa elfu mbili kumi na saba zikamsababishia matatizo si haba, alipoteza kila kitu chake na kumlazimu kurudi nyumbani matunda.

Akiwa matunda aliwahi kukutana na Sadat Mhindi ambaye alimsign kwa label ya maliza umaskini.

Mwaka wa elfu mbili na tisa, Denis alihamia Nairobi ambapo aliendeleza jitihada za kuganga njaa. Maisha jijini yalikuwa magumu sana kwake, aliwahi kulala nje kwa kukosa pesa za kulipia nyumba. Ni katika kipindi hicho ambapo alikuwa karibu kukata tama ya kuendelea na muziki lakini baadae akaghairi nia.

Maisha yalianza kumbadilikia kifedha mwaka wa elfu mbili kumi na nne, mwaka ambao alifanya collabo na Jimmy Gait na kushoot video afrika kusini. Mwaka uliofutia alifanya video na Daddy owen.

Wasanii katika tasnia ya muziki wamekuwa wakipambana kifedha lakini sio Papa Denis. Takriban video zake zote alianza kufanyia nje ya nchi pamoja na kufanya collabo za kimataifa na wasanii kama vile Ray C, Chidinma,  Korede Bello,  Flavour miongoni mwa wengi wengineo. Mavazi yake pamoja na mapambo yalikuwa ya bei, mara suti ya shilingi milioni moja, mara kiatu cha elfu themanini na vitu vinafanana na hivyo.

Mwaka wa elfu mbili kumi na sita aliwahi kudaiwa kuwa ana zaidi ya millioni hamsini ambazo akiongea katika vyombo vya habari alisema kuwa utajiri wake ni zao la muziki. Hata hivyo aliwahi kutaja kuwa kuna watu wengi ambao wamekuwa wakimsaidia kutoka mataifa ya Nje. Je watu hao ni akina nani?

Katika mojawapo ya mahojiano yake ya mwisho, Denis alionekana kama mtu mabaye alikuwa amevurugika, ni katika mahojiano hayo ambapo alitangaza kuwa atahamia marekani si muda mrefu.

Swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza ni je utajiri wa haraka kiasi hicho aliutoa wapi? Na hivi kitendawili cha kifo chako chake kinaweza kuteguliwa na utajiri huo wa haraka au ni sadfa tu?

Katika safari yake ya muziki, papa Denis ameshinda tuzo nne kuu ambazo Mwafaka awards mwaka wa elfu mbili kumi na tano, Pulse Video Awards mwaka wa elfu mbili kumi na sita na elfu mbili kumi na saba, AFRIMMA mwaka wa elfu mbili kumi na nane, na Dear Award mwaka wa elfu mbili kumi na tisa.

Lala pema palipo na wema Papa Denis

 

 

 

Share.

About Author

Leave A Reply