Wasanii wa WCB lavalava na Queen Darling wametia tamko kuhusiana na kitendawili cha Diamond Platnumz na Tanasha Donna kuachana. Wawili hao wamemetaja patashika inayoendelea katika kati ya Diamond na Tanasha katika wimbo unaoenda kwa jina “Bachela”

Wamegusia kuwa ni afadhali kutowahi kuingia kwenye uhusiano kuliko kuwa katika uhusiano au hata ndoa lakini ukaachwa baadae wakizungumzia Tanasha ambaye ameachwa na Diamond platnumz na kuishia ku unfollow takriban wasanii wote wa WCB.

Katika wimbo huo ambao ni mtindo wa gonjera, Queen darling anasifia ndoa huko Lavalava akisema bora kuwa bachela.

 

“Kwanza naona mapenzi faida hayana, Heri niwe Bachela… Queen Darleen acha kunichachafya, heri tu niwe Bachela, Uliza kilichomkuta Dangote, sijui kagombana na Tanasha ametu-unfollow wote … ndo maana nimetulia, navuta pumzi sitaki kwenda mbio, mambo ya kujifanya hodari ati mjuzi…” Aliimba lavalava

Queen Darline anajibu kwa kusema Mapenzi Ya Sikuhizi Shemeji Lokole Muongoza Umbea Mkigombana Tu Kashatease Insta Nzima Imeshaenea BORA NIWE BACHELA… tukiachana na yote mimi bado sikuungi mkono, wasafi wote mnaonekana mnapenda ngono”

Kwa majuma kadhaa uhusiano wa Diamond na Tanasha umekuwa gumzo baada yao kudaiwa kuachana. Tanasha alianza kwa kuanfollow Diamond pekee kisha wasanii walio katika record label ya WCB wakafwatia.

Tanasha hakuachia hapi bali alidondoa maelezo ya Instagram katika ukurasa wa mwanawe sehemu iliosema kuwa “Mtoto wa Diamond” na kubakia maelezo ya mtoto wa Tanasha pekee. Ameahidi kutoa wimbo kuhusu masaibu aliyokutana nayo. Diamond bado hajatoa tamko.

 

Share.

About Author

Leave A Reply