Rais wa marekani Donald Trump ametangaza kusitishwa kwa safari zote za kutoka ulaya kwa takriban siku thelathini. Hili ni kutokana jitihada za kuhakikisha kuwa wanadhibiti virusi vya ugonjwa Korona. Hata hivyo safari za Uingereza hazitasitishwa.

Katika hotuba yake iliyopeperushwa kwa njia ya runinga, Trumph amesema kuwa safari zitasitishwa kutoka saa sita usiku ijumaa.

Trump amesema muungano wa ulaya wamekosa kuchukua tahadhari kama marekani wanavyochukua kuhakikisha kuwa virusi vya corona havisambai.

Kwa sasa marekani imerekodi vifo 1,135 huku 38 miongoni mwao wakiaga dunia.

Virusi vya Korona  (2019-nCoV)  vilitangazwa kwa mara ya kwanza  2019 mwishoni mjini Wuhan, China huku ikikisiwa kuwa ugonjwa huo chimbuko lake ni wanyama (zoonotic disease).

Kwa sasa watu 118,326 wamedhibitishwa kupata virusi vya Korona huku watu 4,292 wakiaga dunia. Nchi ya China inaongoza na kuwa na watu wengi ambao wanaugua ikiwa ni takriban watu 80, 955 huku walioaga dunia wakiwa takriban 3,162.  Visa ambazo zimetangazwa nje ya China ni takriban 37,371 huku 1,130 dwakiaga dunia.

 

Share.

About Author

Leave A Reply