Historia ya Dikteta IDDI AMINI wa Uganda aliyeaminika kula nyama za watu

Afrika kumetokea kuwa na viongozi wakatili, lakini hakujatokea zaidi ya kiongozi mkatili kama Idi Amin Dada.
Idi Amin Dada alikuwa mwanajeshi kutoka nchi ya Uganda aliyepindua serikali na kujifanya rais wa Uganda tangu mwaka 1971 hadi 1979 hadi alipofukuzwa na jeshi la Tanzania. Alitawala kidikteta uchumi wa chi ukaporomoka Watu takriban laki tano wakauliwa na utawala huku wengi wakilemazwa na wengine wakilazimika kukimbilia mataifa ya nje.
Katika miaka yake ya kushika serikali Amin alibadilika kutoka uhusiano wa kirafiki na nchi za magharibi na hasa Israeli kuhamia upande wa Muammar Gaddafi wa Libya, Mobutu Sese Seko wa Zaire, Umoja wa Kisovyeti na Ujerumani ya Mashariki. Hata hivyo Amin alipata usaidizi wa ofisi ya upelelezi ya Marekani CIA iliyotuma silaha na vifaa vingine kwa jeshi lake.

 

Wazungu aisee balaa tupu, raha yao ni afrika tukungatane ili wapate nafasi ya ama kutuibia malia ghafi wakati tukipigana ama watengeneze soko lao kwa kutuuzia silaha.

Mwaka 1977 Amin alivunja uhusiano wa kidiplomasia na Uingereza akajitangaza kuwa alishinda na kujiongezea sifa ya CBE (“Conqueror of the British Empire”). Kuanzia wakati ule cheo chake rasmi kilikuwa “His Excellency President for Life, Field Marshal Alhaji Dr. Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, CBE”.
Alijiona ndume na kuanza harakati za kuvamia mataifa jirani ili kufanya mataifa yaliyomzunguka kuwa miliki ya taifa la Uganda. Huyu bwana aliyeishia darasa la nne aliwahi kutishia kutuchua sehemu zifwatazo za Kenya Turkana, West Pokot, Tranz-Nzioa, Bungoma, Busia, Kakamega, Central Nyanza, South Nyanza, Narok, Kisii, Kericho, Nakuru, Uasin Gishu, Elgeyo, Marakwet, Nyandarua, Nandi, Kisumu, Eldoret, Tambach, Maji Moto, Maji Mazuri, Gilgil, Nakuru, Lake Baringo na Naivasha lakini Rais wa Kenya wa kipindi hicho Jommo Kenyatta akamwambia dhubutu uone moto.
Jaribio la Amin la kutwaa sehemu za Mkoa wa Kagera wa Tanzania mwa ka wa 1978 ilisababisha Vita vya Kagera baina ya Tanzania na Uganda na mwisho wa utawala wake. Amin alikimbia kukaa ugenini Libya na baadaye Saudia alipoishi hadi kifo chake mwaka 2003.

 

Huyu bwan alizaliwa wapi?

Hakuna uhakika juu ya mwaka na mahali alikozaliwa. Amin mwenyewe hakuandika kumbukumbu ya maisha yake wala hakuagiza taarifa rasmi juu ya maisha yake ziandikwe. Vyanzo mbalimbali vinasema ya kwamba alizaliwa mnamo 1925 Koboko au Kampala. Mtafiti Fred Guweddeko amedai Amin alizaliwa 17 Mei 1928, lakini hii imepingwa na wanawe Amin Hussein ambaye anasema babake alizaliwa Kampala mwaka 1928.

kulingana na Fred Guweddeko wa Chuo Kikuu cha Makerere, Idi Amin alikuwa mwana wa Andreas Nyabire ambaye alizaliwa mwaka wa elfu moja mia nane themanini na tisa na kufariki mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na sita. Nyabire alikuwa wa kabila la Wakakwa, Mkatoliki aliyehamia Uislamu mnamo 1910 akibadilisha jina lake kuwa Amin Dada na kumpa mwana wa kwanza jina hilo pia.

Iddi Amin alilelewa na mama yake bila baba kijijini Kaskazini-magharibi mwa Uganda. Kufuatana na Gudewekko mamake Amin Assa Aatte aliyeishi kati ya mwaka wa elfu moja mia tisa na nne na elfu mojha mia tisa na sabini alikuwa Mlugbara aliyetibu watu kwa mitishamba. Amin alisoma miaka kadhaa kwenye shule ya Kiislamu huko Bombo kuanzia mwaka 1941.

Baada ya miaka michache ya shule na kazi ndogondogo aliajiriwa mwaka 1946 na afisa Mwingereza wa jeshi la kikoloni King’s African Rifles (KAR).

Aliingia jeshini huko Jinja akifanya kazi ya msaidizi jikoni akiendelea kupokea mafunzo ya kijeshi. Baadaye Amin alidai ya kwamba alilazimishwa kuhudumia huko Burma katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mwaka 1947 alihamishiwa Gilgil, Kenya. Mwaka 1949 alitumwa kaskazini kupigana na waasi Wasomalia. Tangu mwaka 1952 kikosi kilipigana na wapiganiajiaji wa uhuru waliofahamika kama Maumau karibu na Mlima Kenya.

Aliendela kupanda vyeo vilivyopatikana kwa Waafrika katika jeshi la KAR na muda mfupi baada ya uhuru alipewa cheo cha luteni yaani afisa kamili kama mmoja wa Waganda wawili. Baada ya uhuru wa Uganda mwaka 1962 alikuwa kapteni halafu mwaka 1963 meja. Mwaka 1964 alikuwa makamu wa mkuu wa jeshi na mwaka 1965 mkuu wa jeshi, mwaka 1970 mkuu wa shughuli zote za kijeshi.
Amin alipandishwa cheo na waziri mkuu Milton Obote baada ya uasi wa wanajeshi katika Afrika ya Mashariki wa 1964 uliokomeshwa na askari Waingereza katika Tanganyika, Kenya na Uganda akawa makamu wa mkuu wa Jeshi aliyekuwa bado Mwingereza. Kutoka hapa alishirikiana na Obote katika hatua za kuimarisha utawala wa waziri mkuu. Wakati bunge la Uganda lilitaka utafiti kuhusu mashtaka ya Obote kushiriki katika biashara ya siri ya pembe za ndovu kutoka Kongo Obote aliamua kubadilisha katiba na jeshi la Amini lilimfukuza Mkuu wa Dola Kabaka Mutesa kwa nguvu, halafu Obote alijitangaza kuwa rais. Sasa Amin akawa kanali na Mkuu wa Jeshi.

Amin alianza kuajiri hasa askari kutoka kaskazini mwa Uganda mpakani mwa Sudani.

Mwaka 1970 Obote aliendelea kumpa Amin cheo cha mkuu wa mikono yote ya jeshi na ulinzi. Lakini Amin alisikia pia ya kwamba kulikuwa na mashtaka dhidi yake kutokana na matumizi ya makisio ya jeshi na mipango ya Obote kumfanyia utafiti. Hapo Amin alitumia nafasi ya safari ya Obote kwenda nje kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Madola, akatwaa mamlaka ya serikali tarehe 25 Januari 1971.

Mara moja alianza kuwatesa wafuasi wa Obote na watu wote waliompinga. Kuna makadirio ya kwamba jumla ya watu 100,000 hadi 500,000 waliuawa katika miaka minane ya utawala wake.

Aliharibu uchumi wa Uganda kwa ufisadi na majaribio ya kuongoza biashara. Hatua kubwa ya uharibifu ilikuwa kufukuza watu wote wenye asili ya Kihindi na kugawa maduka na biashara yao kwa ndugu au wafuasi wa rais. Takriban watu 80,000 walipaswa kuondoka kwao wakihamia Uingereza, Marekani au Kanada.

 

Kwa ushirikiano na mkuu wa jeshi Maliyamungu walitesa, wakaua na kulemaza wengi. Yule bwana alikuwa hambiliki hasemezeki, ukimkosoa ndo umebusu kifo.

 

 Kay Amin ambaye alikuwa mke wake wa nne kati ya wake watano aliwahi kupatikana akiwa amekatwakatwa ikiaminika kuwa aliuliwa na Amini kwa kuhusishwa na madai ya kuchepuka na daktari wake.

Ndio raisi wa pekee mwafrika au hata mwafrika wa kipekee kwa jumla kuwahi kubebwa na wazungu. Amin alifanya hivyo kuondoa kiburi cha ukoloni.

Alijipa vyeo vingi, vikiwemo Field Marshall, Al Hadj, Doctor Idi Amin Dada! (Ajabu, daktari aliyeishia darasa la nne) Inasemekana alimtumia malkia wa uingereza Elizibeth II barua za kimapenzi akimuomba amuoe ili aweze kujiita mfalme kwani alikuwa ameshajipa vyeo vyote kasoro “King” Yaani mfalme

Mnamo Oktoba 1978 Amin alianzisha vita dhidi ya Tanzania kwa kuvamia sehemu za mkoa wa Kagera. Rais Julius Nyerere wa Tanzania aliamua kumwondoa Amin kabisa na jeshi la Tanzania likatwaa Kampala tarehe 11 Aprili 1979.

Amin alitorokea Libya, halafu Irak na mwishowe Saudia alikopewa kimbilio kwa masharti ya kutoshughulikia siasa tena.

Alikufa mjini Jeddah tarehe 16 Agosti 2003.

Je ni Kweli Iddi Amini Alikuwa Akila Nyama za Watu?

Hili bado ni swali ambalo halina majibu, ila watu mbali mbali wanaamini kuwa alikuwa akila huku baadhi ya watu wakipinga.

Chavez, Rais wa Venezuela, aliwahi  kudai kuwa rais wa zamani wa Uganda Idi Amin hakuwa muuaji na mla nyama za watu kama inavyosemekana.
“Tulifikiria kuwa Amin ni muuaji mla nyama za watu” Chavez alisema alipokuwa akimuongelea Idi Amin ambaye anatuhumiwa kuwaua maelfu ya wapinzani wake wakati wa utawala wake nchini Uganda kwenye miaka ya 1970.

“Nina shaka kama Idi Amin alikuwa muuaji kama inavyosemekana, badala yake alikuwa mwanaharakati mtetezi wa nchi yake”, alisema Chavez.

Mary Karoro Okurut, msemaji wa chama tawala cha Uganda akizungumzia kauli hiyo ya Chavez alisema kuwa mtu yoyote anayedhania kuwa Idi Amin alikuwa ni mtu mwema atakuwa na matatizo ya akili.

“Idi Amin alikuwa ni mtu mkatili ambaye aliua raia wengi wa Uganda na kisha kukimbilia nje ya nchi. Mtu yeyote anayemtetea Amin atakuwa na matatizo”.

Naye sekretari wa rais Yoweri Museveni, Tamale Mirundi, alielezea rekodi ya Idi Amin ya kuwaua wapinzani wake akiwemo mmoja wa wake zake.

“Kama unamuoa mwanamke na kisha baadae unamuua, huwezi kuitwa mume mzuri”, alisema na kuongeza “Hivyo ndivyo alivyofanya Amin, aliwaua raia wengi wa Uganda hawezi kuitwa mtetezi wa nchi”.

Kumekuwa na mitazamo tofauti kuhusiana na Idi Amin baadhi ya watu wakiamini kuwa ukatili anaotuhumiwa kuufanya zilikuwa ni propaganda za kumchafua huku watu wengi wakiendelea kuamini kuwa Idi Amin ndiye mhusika mkuu kwa mauaji ya watu 500,000.

Miongoni mwa mambo ya kikatili ambayo Idi Amin anatuhumiwa kuyafanya ni kuwaua watu na kula nyama zao na kuhifadhi nyama za watu kwenye majokofu.

 

 

 

Share.

About Author

Leave A Reply