Baada ya kifo cha marehemu John De Mathew jamii ya Agikuyu walisikika wakisemakuwa jamii hiyo imebaki na na nabii mmoja ambaye ni Muimbaji Muigai wa Njoroge na ambaye kila kukicha ameendelea kudhihirisha kuwa cheo cha unabii kinamfaa.

Muigai katika siku za hivi karibuni ametoa tamko ambalo limekuwa gumzo mitaani. Kupitia account yake ya youtube amewasilisha ujumbe kwa lugha ya Kikuyu ITONGA CITU CIHA, KENYA NITURI ITONGA? Tafsiri yake ikiwa matajiri wetu wako wapi , ama hatuna matajiri Kenya?

Ameanza kwa kusema kuwa katika jamii kuna watu watatu muhimu ambao ni shujaa, tajiri na kiongozi.

Shujaa mchango wake huonekana wakati jamii imevamiwa na adui na hapo ndipo mashujaa hujitolea kupigania jamii.

Kiongozi kazi yake ni kuongoza watu ilhali tajiri kazi yake ni kusaidia jamii haswa kwa chakula wakati ukifika wa watu kutokuwa nguvu na ama uwezov wa kujitafutia kutokana na majanga.

Muigai ameendelea kusema majukumu ya shujaa na kiongozi yamekuwepo lakini jukumu la tajiri halijawahi kuwepo hadi corona ilipobisha hodi.

Kutokana na kuwa watu wameombwa kukaa nyumbani ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona, amerai matajiri wajitokeze kusaidia masikini kwa kuwa kuambia masikini akae nyumbani ni sawa na kumuua na njaa.

Kando na njaa kuwa baa kubwa zaidi ya corona, ameeleza kuwa kuna watu ambao hawana hata maskani ya kuita nyumbani, wako na kibanda tu cha kumsitiri kiza ndo kesho yake aamke kutafutia watoto.

Ameomba matajiri wote wakiwemo Rais Kenyatta, Kabogo, Mama Ngina, Chandaria, Jimmy Wanjigi junior miongoni mwa wengi wengineo wajitokeze kusaidia.

Amerai serikali kutupilia mbali bili za maji na umeme na kuongea na wenye nyumba za kukodisha kusitisha uchukuaji wa kodi hadi janga la corona liondoke.

Amemalizia kwa kusema kuwa jitihada za kusaidia masikini zisipofanyika wakati watu wanaendelea kuambiwa wakae nyumbani, njaa ikiwalemea sana wataanza kujichukulia wenyewe akitilia mkazo  maneno ya wahenga wengi wape na usipowapa watajichukulia wenyewe.

Je, Hapo ulipo yanayachukuliaje maneno ya Muigai wa Njoroge?

Share.

About Author

Leave A Reply